Askofu kakobe aeleza kuhusu pete ya ndoa

Maelezo ya Askofu kakobe kama alivyoulizwa na mwandishi wa habari.
Mwandishi:
Kuna waliosema kuwa ulianzisha kanisa nchini Marekani na ulikuwa na mpango wa kuhamia huko, je ni kweli?
Askofu Kakobe:
Kuhama nchi siwezi lakini ni kweli baada ya maombi ya muda mrefu Aprili 16, 2012 nilifungua kanisa Marekani, hii ni nia ileile ya kuokoa mataifa na kuinua jina la Yesu.
Mwandishi:
Tunaona watu wakifunga ndoa wanavaa pete lakini katika kanisa lako hilo halipo, unazungumziaje hilo?
Askofu Kakobe:
Pete kwenye ndoa siyo agizo la Bwana na ndiyo maana tunaona Mungu mwenyewe akichukizwa na watu waliovaa pete, vikuku na mapambo mengineyo. Soma maandiko haya Isaya 3:21, 16-24; Hosea 2:13; Mwanzo35:1-5; Kutoka 33:4-6; Yeremia 4:30; 1Timotheo 2:9-10; 1Petro 3:3-5. Mapambo ni mavazi ya waabudu miungu, yanahusishwa na ibada ya miungu (mashetani).
Mwandishi:
Lakini wanaotumia pete katika ndoa wanasema eti pete ni mfano wa upendo usio na mwanzo na mwisho, unasemaje kuhusu madai hayo?
Askofu Kakobe:
Hiyo siyo kweli, mwanzo wa upendo ni pale walipokutana na wakapendana na mwisho wa upendo ni pale mmoja anapofariki na kumfanya mwenzake kuwa huru kuolewa au kuoa. Yesu alisema mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa. Hutapewa mke wako au mume wako uishi naye huko mbinguni. Yote hii ni janjajanja ya shetani anayekuja kwa mfano wa malaika wa nuru ili kutufanya tuingize mapambo katika nyumba ya Mungu na kujenga ngome za mashetani kwa visingizio kwamba mimi nimevaa pete sasa ni mke wa mtu au mume wa mtu. Mbona nyumba za wageni (guest houses) zimejaa watu wenye pete za ndoa? Kama pete hizo zingekuwa zinawafanya watu wasiwe makahaba, tusingekuwa na matatizo tuliyonayo leo.
Askofu kakobe aeleza kuhusu pete ya ndoa Askofu kakobe aeleza kuhusu pete ya ndoa Reviewed by gwamaka on 10:34:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.