Bwana Yesu Asifiwe!!Tunaendelea tena leo kukuletea mfululizo wa nguvu zilizomo na uwezo uliomo katika Damu ya Yesu Kristo.
Mathayo 27:29inatuambia ya kuwa Yesu alivikwa “taji ya miiba” kichwani pake; na “wakamdhihaki, wakisema, salamu, Mfalme wa Wayahudi”.
Waliomsulubisha walipokuwa wanamdhihaki katika tendo hilo, hawakujua kwa Damu ya Yesu iliyomwagika wakati huo, ilikuwa inaandaa mazingira ya watakaomwamini kufanyika wafalme!
Hii ni kwa sababu “taji” ni sehemu ya vazi la kifalme! Ufunuo wa
Yohana 5:9,10inatuambia ya kuwa juu ya Yesu: “Ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi”.
Tafsiri za biblia za kiingereza zinasema “Ukawafanya wafalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi”. Kwa hiyo, kama unamwamini Yesu na umeokoka, umefanyika mfalme katika Yeye. Je, unalijua hili? Na je, unaliamini kwa kiwango kipi? Je, unajua kuishi na kutawala kama mfalme katika ulimwengu huu maana yake nini?
(Warumi 5:17).
Source Christopher & Diana Mwakasege (Mana ministry) Facebook page
Reviewed by gwamaka
on
11:49:00 PM
Rating: