Nani aligawanya vitabu vya biblia katika vifungu na mistari? kwa nini na lini alifanya hivyo?
JIBU:
Hapo mwanzo biblia ilipoandikwa haikuwa imegawanywa katika vifungu/mlango na mistari iliyopo sasa.Biblia iligawanywa katika milango na mistari ili kusaidia uwezo wa kutafuta na kusoma neno kwa urahisi.
kwa sababu ni kazi rahisi kutafuta "yohana mlango wa 3, mstari wa 16" kuliko kutafuta "kwa mana jinsi hii mungu aliupenda....". Japokuwa sehemu chache, milango/vifungu vimekatwa vibaya bila kuzingatia milango ambayo inamuendelezo. Lakini yote katika yote vifungu na mistari inasaidia sana katika biblia.
Vifungu vya biblia tunavyovitumia sasa viligawanywa na Stephen Langton, Askofu wa Canterbury.
Langton aliweka vifungu hivi kwenye Biblia mnamo miaka ya A.D. 1227. Biblia ya Wycliffe English ya 1382
ndiyo ilikuwa biblia ya kwanza kugawanywa kwenye vifungu /milango. Kutoka Biblia ya Wycliffe, karibia
tafsiri za biblia zote zimefuata mfumo wa vifungu uliowekwa na askofu Langton's.
Agano la kale la kiyunani liligawanywa kwenye mistari na Myahudi rabbi kwa jina la Nathan in A.D. 1448. Robert Estienne, ambaye pia alijulikana Stephanus, ndiye alikuwa wa kwanza kuligawa agano jipya katika mistari ya namb, mnamo mwaka 1555. Stephanus alitumia sana staili ya Nathan alivyoigawa agano la kale.
kutokea muda huo, ukianzia na biblia ya geneva, mtindo wa vifungu na mistari uliowekwa na Stephanus umetokea
kukubalika karibia na aina zote za biblia.
Nani aligawanya vitabu vya biblia katika vifungu na mistari? kwa nini na lini alifanya hivyo?
Reviewed by gwamaka
on
1:08:00 AM
Rating:
No comments: